1. main content
  2. main navigation
  3. extra content
  4. head navigation
  5. search
  6. Choose form 30 Languages

 
 
 

 

 | 08.01.2009 | 03:00 UTC

Israeli imeanzisha upya mashambulio ndani ya Ukanda wa Gaza  baada ya saa tatu za utulivu kumalizika.





Urusi yatoa masharti mapya kabla ya kurudisha gesi kwa nchi ulaya kupitia Ukraine.




Serikali ya Zimbabwe yasema waandishi wa habari wa kigeni nchini humo watahitajika kulipa hadi dolla elfu 30 kupata kibali cha kufanya kuendesha shughuli zao nchi humo.

Mashambulio ya Israel yaaanza tena baada ya kusimamishwa kwa saa Tatu

Gaza


Wanajeshi wa Israeli wameanzisha upya mashambulio baada ya kumalizika  saa tatu za utulivu kutoa nafasi kwa misaada ya kiutu kuingia Gaza.Misaada ya mbali mbali iliingizwa Gaza hapo jana wakati wa kipindi hicho .Hatua ya Israeli ya kusimamisha vita kwa saa tatu kila siku imepongezwa na mashirika ya kutoa misaada katika Gaza.John Ging  mkuu wa shirika la misaada la Umoja wa mataifa UNRWA anasema wameridhia hatua hiyo kama hatua ya kwanza ingawa sio suluhisho na pia wanatumai kwamba itakuwa ni muda wa saa tatu utakaotoa usalama kwa watu milioni moja na nusu wa Gaza.Kwa upande mwingine juhudi za kidiplomasia zinaendelea lakini baraza la usalama la Umoja wa mataifa limeshindwa kukubaliana juu ya hatua ya kumaliza mzozo huo lakini Marekani imetangaza kuunga mkono mpango uliopendekezwa na Misri na Ufaransa wa kusitisha mapigano.Misri itaandaa mazungumzo na pande zote mbili Israel na Hamas juu ya pendekezo hilo.Ujerumani pia imekubaliana na pendekezo la rais Hosni Mubarak juu ya kusimamishwa vita kati ya Hamas na Israeli.Aidha waziri wa mambo ya nje Frank Walter Steinmeir amepongeza hatua ya Israeli ya kutoa nafasi ya kupelekwa misaada ya kiutu katika ukanda wa Gaza.Kwa upande mwingine wanasiasa wa ngazi ya juu kutoka vyama vyote vya serikali ya muungano wameonyesha nia ya kuridhia jeshi la kuweka amani la Ujerumani kulinda amani Gaza ikiwa kutafikiwa makubaliano ya kusitisha vita  chini ya azimio la Umoja wa mataifa.Hata hivyo msemaji wa serikali ya Ujerumani amesema kuwa ni mapema mno kuzungumzia suala hilo.

Kwa mujibu wa taarifa za hospitali katika Gaza watu zaidi ya 700 wameuwawa  na wengine 3000 wamejeruhiwa hadi sasa tangu Israeli ilipoanzisha mashambulio dhidi ya Hamas.

Urussi yaahidi kusambaza gesi kwa njia za ulaya

Moscow


Rais wa Urusi Dmitry Medvedev ametoa masharti mapya ya kurudisha gesi kwa nchi za Ulaya kupitia mabomba ya Ukraine.Medvedev amemwambia rais wa Ukraine Viktor Yushenko kwamba Kiev inabidi kukubaliana na kiwango cha bei ya gesi ya Urusi na kulipa madeni yaliyosalia pamoja na kuruhusu waangalizi wa Umoja wa Ulaya ili kuthibitisha usafirishaji wa gesi kupitia mabomba ya nchi hiyo.Rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya  Jose Manuel Barosso akizungumzia kuhusu mzozo huo amesema haiwezi kukubalika kwamba gesi inazuiwa kufika nchi za Ulaya  kutokana na mvutano wa nchi mbili Urusi na Ukraine. Amesema kwa nchi za Bulgaria,Slovakia na nyingine za Umoja wa Ulaya muhimu sio mzozo umenzishwa na nani Urusi au Ukraine tatizo ni kwamba gesi kutoka kampuni ya Gazprom haifiki kwenye nchi za Ulaya.

Mazungumzo ambayo yanadhaminiwa na Umoja wa Ulaya kati ya Urusi na maafisa wa masuala ya nishati kutoka Ukraine yamepangiwa kufanyika hii leo mjini Brussels Ubelgiji.Kiasi kikubwa cha mahitaji ya gesi asili katika Umoja wa Ulaya kinatoka Urusi.

Makampuni yanayoyumbayumba kiuchumi kupigwa jeki

Berlin


Serikali ya Ujerumani ina mipango ya kutoa msaada wa hadi euro billioni 100 kwa makampuni ya humu nchini ambayo yanakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi.Hayo ni kwamujibu wa mwanasiasa wa ngazi ya juu kutoka upande wa wahafidhina Volker Kauder.


Kiongozi huyo wa kundi la wabunge wa vyama ndugu vya CDU CSU mjini Berlin amesema hapo jana kwamba msaada huo utatolewa kwa makampuni yanayokabiliwa na matatizo ya kupata mikopo kutoka mabenki na yanayoshindwa  kupata mtaji kwenye masoko ya fedha.Serikali ya Ujerumani tayari imetoa euro billioni 400 kuzisaidia benki za humu nchini ambazo zinamatatizo ya fedha kutokana na mzozo wa kiuchumi duniani.

Zimbabwe yatangaza vikwazo vipya kwa waandishi wa kigeni

Harare



Serikali ya Zimbabwe imetangaza kwamba waandishi wa habari wa kigeni watahitajika kulipa hadi dola elfu 30 kwa ajili ya kupata leseni mpya ya kuendesha shughuli zao nchini humo.Hatua hiyo imezusha malalamiko mengi  kwamba serikali inajaribu kuwafukuza waandishi nchini humo.


Sheria hiyo mpya ya Zimbabwe inawataka pia wazimbabwe wanaofanyia kazi mashirika ya habari ya kigeni  kulipa dolla elfu 4000 ili kuendesha shughuli zao kwa kipindi cha mwaka mmoja.Wanasheria  wa kutetea haki za binadamu pamoja na  makundi ya vyombo vya habari barani Afrika kama vile taasisi ya vyombo vya habari ya Afrika Kusini MISA imeanza kutilia wasiwasi  uhalali wa sheria hiyo.


Zimbabwe inatajwa kuwa nchi yenye baadhi ya masharti  magumu kabisa kwa waandishi wa habari duniani  tangu ilipopitisha  sheria inayosimamia utoaji wa habari  mwaka 2002.Waandishi wengi wa habari wakigeni pamoja na wazimbabwe wamekamatwa nchini humo kutokana na kuendesha shughuli zao bila ya kibali tangu sheria hiyo ilipotazangazwa.

Mvutano wa India na Pakistan

Mumbai

Serikali ya India imesema kuwa nakala za simu zilizonaswa  zinaonyesha kuwa wanamgambo wakiislamu walioshambulia mji wa Mumbai mwezi Novemba  walikuwa wakipata muongozo kutoka Pakistan.


India imewasilisha ushahidi wake kwa Pakistan ambao inadai kwamba magaidi wanaendesha shughuli zao kutokea Pakistan. Hata hivyo serikali ya mjini Islamabad imekanusha tuhuma za waziri mkuu wa India Manmohan Sighn kwamba mashambulio ya Mumbai yalikuwa yakiungwa mkono na maafisa  wa idara ya upelelezi ya Pakistan.Pakistan  lakini imethibitisha hapo jana kuwa  gaidi  pekee aliyenusurika na kukamatwa na maafisa wa India ni raia wa Pakistan.

Idadi ya watu wasio na ajira nchini Ujerumani yapanda

Berlin


Kitisho cha ukosefu wa ajira duniani kimeongezeka baada ya hapo jana kutolewa ripoti juu ya tatizo hilo.Kwa mara ya kwanza  tangu mwezi wa Februari mwaka 2006  Nchini Ujerumani idadi ya watu wasio na Ajira imeongezeka katika mwezi wa Desemba.


Hali hii inaonyesha ni jinsi gani mzozo wa fedha duniani ulivyoathiri makampuni  katika nchi zenye uchumi imara barani ulaya. Idadi ya wasiokuwa na ajira Ujerumani ni kubwa kabisa kuliko ilivyotarajiwa.Ripoti iliyotolewa na ofisi ya masuala ya kazi imekuja wakati ambapo wabunge wa Ujerumani wameanza kushughulikia mpango wa  pili wa kuupiga jeki  uchumi wa ndani ambao huenda ukafikia  euro billioni 50 zaidi.



 
Picture of the Day
ImageOfTheDay

DW-TV EUROPE live

Journal (deutsch) - Mit Tagesthema